Skuli zote zilifungwa wiki iliyopita kwa ajili ya mapumziko ya
Novemba – Desemba ambapo zinatarajiwa kufunguliwa Januari 2, 2019.
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Paul Kibet alisema, Wizara imetoa
mapumziko hayo ili kuwawezesha wanafunzi kuweza kujipumzisha na
kujichanganya na jamii, sambamba na kuungana na familia zao na jamii
ambazoo wanatokea.
“Ndio maana skuli zinashauriwa kutowapa wanafunzi wao kazi nyingi
wanapokwenda nyumbani kwa ajili ya mapumziko.
Iwapo watapewa kazi hizo
wakiwa katika mzingira ya nyumbani itawazuia kujichanganya na maisha
kikamilifu,” alisema Kibet.
Zanzibarleo.
Comments