Aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando
ameshindwa kuulizwa maswali na upande wa mashtaka katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jana baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kutokuwepo mahakamani hapo.
Wakili
Swai ambaye anaiwakilisha Serikali kwenye kesi hiyo, ilielezwa
mahakamani hapo yupo safarini Musoma mkoani Mara kwa shughuli nyingine
ya kikazi.
Wakili
wa Takukuru, Dismas Muganyizi, alieleza mahakamani mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Wakili Swai yupo nje ya Mkoa wa Dar es
Salaam na amekwenda Musoma kwenye majukumu mengine na kuiomba mahakama
hiyo kuahirisha kesi hiyo.
Hata
hivyo, Tido alitakiwa kuulizwa maswali dhidi ya utetezi alioutoa
mahakamani hapo Septemba 20, mwaka huu huku akiongozwa na mawakili wake,
Dk. Ramadhani Maleta na Martin Matunda.
Hakimu
Shahidi aliridhia ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo
hadi Oktoba 30, ambapo Tido ataanza kuulizwa maswali na upande wa
mashtaka dhidi ya utetezi wake.
Katika
kesi hiyo, upande wa mashtaka ulileta mashahidi ambao ni pamoja na
aliyekua Mkurugenzi wa Shirika hill, Clement Mshana, Ofisa uchunguzi wa
Takukuru, Victor Lesuya na Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa.
Tido alisomewa mashtaka manne likiwamo la kutumia madaraka vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.
Mpekuzi.
Comments