Vijana wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuonyesha uthubutu katika kujiajiri kwa kuzithamini kazi wazofanya.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi na Ajira, Anthony Mavunde, wakati wa ufunguzi wa wiki ya vijana
kitaifa inayofanyika katika viwanja vya Tangamano, Jijini Tanga.
Amesema
vijana wanatakiwa kuzithamini shughuli wanazofanya kwa kuzipa
kipaumbele ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya
kuajiriwa.
“Vijana
muondokane na mawazo mgando kutegemea kuajiriwa badala yake wajikite
katika kujiajiri na Serikali itawapa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji
na kuboresha mazingira ya shughuli mnazofanya,” amesema Mavunde.
Katika
hatua nyingine Waziri mavunde amewataka vijana kujitokeza kwa wingi
katika sherehe za kilele cha mbio za mwenge zitakazofanyika Oktoba 14,
katika viwanja vya Mkwakwani, mjini hapa.
Mpekuzi.
Comments