Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linaendelea kuwashikilia
wafanyakazi wanane wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART) akiwamo
kigogo wa idara wa fedha ambao wanadaiwa kuhusika katika mtandao wa
uhujumu wa mapato ya mabasi ya mwendokasi kwa kuchapisha tiketi feki kwa
abiria.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa jana, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa watuhumiwa hao
wanaendelea kuhojiwa huku wengine 18 wakiachiwa kwa dhamana.
Alisema upelelezi utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi.
“Bado
tunawashikilia watuhumiwa wanane ambao walishiriki moja kwa moja tukio
hilo huku wengine 18 ambao walishiriki kwa mbali tumewapa dhamana wakati
tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Mambosasa.
Kamnada
Mambosasa alisema, watuhumiwa hao wamefanya kosa hilo la kuhujumu mradi
wa Serikali ambao ni wa kitaifa na kimataifa kwa kutaka kufifisha
jitihada za Serikali.
“Mradi
huu unalitangaza Jiji la Dar es Salaam na taifa kwa ujumla kimataifa
hivyo kwenda kinyume na jitihada hizo za serikali ni sawa na uhujumu
uchumi, upelelezi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani
haraka iwezekanavyo,” alisema Mambosasa.
Pamoja
na hali hiyo alitoa tahadhari kwa Kampuni ya Udart, kuwa makini wakati
wa kutoa ajira na kuwataka kufuata vigezo muhimu ili kuepuka kuajiri
watu wasiokuwa na sifa.
Taarifa za kna zinaarifu kuwa wafanyakazi hao kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi , waliunda mtandao maalumu wa kufyatua tiketi feki na kujipatia mamilioni ya fedha.
Mradi huo wakati unaanza mwaka 2016, ulikuwa unabeba abiria 75,000 na kwa sasa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 200,000 na kwa kila safari hulazimika kulipa Sh 650 ukijumlisha kwa idadi hiyo mapato kwa siku yaliyokuwa yanakusanywa hufikia Sh milioni 130,000 ingawa kwa sasa yameshuka.
Katika mtandao huo imebainika mbali ya kufyatua tiketi feki pia wamekuwa wakifanya ujanja kwa kuwauzia watu wazima tiketi za wanafunzi ya Sh 200 badala ya Sh 650 huku kiwango kinachobaki kikingia katika mifuko ya wajanja.

Mpekuzi.
Comments