Ujenzi wa nyumba hizo 30 utagharibu dola za Marekani 987,237,32.
Mkurugenzi wa kukabiliana na maafa Zanzibar, Makame Haji Makame, aliyasema hayo ofisini kwake Maruhubi.
Alisema ujenzi huo kwa sasa unaendelea kwa awamu ya kwanza ambapo nyumba 30 zinaendelea na ujenzi.
Aidha awamu ya pili ya ujenzi huo itaendelea baada ya kumalizika hatua ya kwanza ya ujenzi.
Alisema ujenzi wa awamu ya pili utahusisha skuli ya vyumba saba, maduka 15, kituo cha afya, msikiti, soko na uwanja wa kuchezea watoto.
Alisema lengo la kujengwa nyumba hizo ni kuwaondoshea usumbufu wananchi wanaopata maafa ya nyumba zao kuanguka au kujaa maji pale mvua zinaponyesha.
Alisema mwaka 2017 nyumba 6,005 ziliathirika na mvua hivyo kujengwa nyumba hizo kutaondosha usumbufu kwa wananchi.
Alisema uzoefu unaonyesha kila ifikapo kipindi cha mvua baadhi ya wananchi huhama nyumba zao na kutafuta makaazi ya muda, hivyo kujengwa nyumba hizo kutawaondoshea usumbufu wananchi.
Kuhusu changamoto zilizojitokeza kwa ujenzi wa nyumba hizo, alisema ni tatizo la maji ambapo wajenzi hutumia gari la kampuni hiyo badala ya kuchimba kisima katika eneo la ujenzi kutokana na kuwa maji yanayochimbwa maeneo hayo huwa na chumvi.
Hata hivyo, aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwani nyumba hizo ni mradi wa wao.
Ujenzi wa nyumba hizo, unasimamiwa na mshauri elekezi kampuni ya Samkay Consult Cooperation Ltd ya Dar es Salaam, Amour Hamad Omar, kwa kushirikiana na serikali.
Zanzibarleo.
Comments