Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umelaani wananchi
kuwashambulia na kuwaua askari watatu wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mratibu wa mtandao huo,
Deogratias Bwire, imeeleza kitendo hicho ni cha kikatili dhidi ya
Polisi.
“Kwa
mujibu wa taarifa tulizonazo, polisi watatu akiwemo Mkuu wa Kituo cha
Polisi cha Nguruka (Ramadhani Mdimi), Uvinza mkoani Kigoma
walishambuliwa vibaya na wananchi waliokuwa na silaha za jadi na
kusababisha vifo vya askari hao,” imesema taarifa hiyo.
Amesema
THRDC inafanya kazi kama mwamvuli wa watetezi wa haki za binadamu
nchini imekuwa mstari wa mbele katika kutambua na kutetea haki za
Watetezi wa Haki za Binadamu wakiwamo polisi.
Pamoja
na mambo mengine, amesema jitihada zimekua zikifanywa na THRDC katika
kutambua, kuwatetea na kuwalinda askari wetu wanaofanya kazi kubwa ya
kuwalinda raia na mali zao.
“Mtandao
unapenda kutoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Siro,
Jeshi la Polisi kwa ujumla, ndugu wa marehemu na Watanzania wote kwa
kupoteza nguvu kazi ya taifa,” amesema.
Mpekuzi.
Comments