Serikali imewataka wazalishaji wa zao la muhogo nchini kuongeza uzalishaji ili kuwawezesha kupata soko la uhakika nchini China.
Hatua
hiyo itaifanya Tanzania kuongeza wigo wa kusafirisha zao hilo nchini
humo ambapo kwa mwaka 2017 inakadiriwa kupeleka bidhaa zenye thamani ya
Dola za Marekani laki tatu sawa na Sh.milioni 687, huku China ikiingiza
bidhaa zake hapa nchini zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.1.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa
Siza Tumbo katika mkutano wa wadau wa wa zao la Muhogo kitaifa ambao
umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI), Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki(IITA) na Wizara ya Kilimo, kitengo cha
Mpango wa Maendeleo ya sekta ya kilimo awamu ya pili(ASDP II).
Mkutano huo unalenga kuandaa mipango ya kuendeleza zao hilo kuwa kibiashara na kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Alisema
kama Taifa kunatakiwa kuwapo na msimamo wa kuchangamkia soko la zao
hilo nchini China kutokana na fursa ya kibiashara iliyopo.
“Uzalishaji
upo chini kitakwimu lakini kuuhalisia haipo hivyo, sasa tunatakiwa tuwe
ma champion kwenye uzalishaji wa zao hili ni zuri sana ili tuweze
kuleta mageuzi kwenye zao hili,”alisema.
Alibainisha
kuwa zao hilo nchini ni la pili kwa umuhimu zaidi katika mazao ya
chakula baada ya mahindi na asilimia 84 ya jumla ya uzalishaji nchini ni
kwa matumizi ya chakula cha binadamu, lakini uzalishaji huo bado uko
chini na zao hilo halijatumika kikamilifu.
Aidha
aliwataka Watanzania kula vyakula vya asili ili kulinda afya zao kwa
kuwa kumekuwapo na mtazamo hasi kwa jamii kuwa kuna baadhi ya mazao
ikiwamo muhogo na mtama kwamba hayafai kwa chakula jambo ambalo ni
upotoshaji.
Aliwataka
wakulima wa muhogo kutokatishwa tamaa na kauli hizo badala yake
waongeze nguvu katika uzalishaji ili waweze kushindana na masoko makubwa
ikiwamo nchi ya China.
Tanzania
ni nchi ya 12 kwenye uzalishaji mkubwa wa muhogo duniani na ya sita
barani Afrika baada ya Nigeria, Kongo DRC, Ghana, Angola na Msumbiji
ambapo kila mwaka unachangia asilimia 5.5 ya jumla ya uzalishaji wake
duniani na asilimia 14 kwa Afrika.
Mahitaji
ya baadaye ya zao la muhogo nchini Tanzania unalengwa kuongezeka na
kuwa kati ya tani 530,000 na 630,000 na kwamba hali hiyo inatokana na
kuongeza thamani ya muhogo kwa kutengenezea unga, wanga na kuwa
malighafi katika viwanda vya bia, pipi na vitafunio, viwanda vya nguo,
karatasi, rangi na dawa.
Mpekuzi.
Comments