Serikali kuibua vyanzo vipya vya mapato.

WAZIRI wa Fedha na Mipnago, Dk. Khalid Salum Mohammed, amesema wizara imepanga kufanya utafiti wa kina wa vyanzo vya mapato vilivyopo na kuibua vyengine.
Aliyasema hayo alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa maoni na ushauri wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2018/2019, Chukwani.
Alisema utafiti huo utasaidia upangaji wa bajeti ya mwaka 2019/2020 na kuwa na makisio katika vyanzo vya mapato.
Kuhusu mradi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume (termina III) na bandari ya Mpigaduri, alisema suala hilo linalishughulikiwa ambapo hivi karibuni watakaa kuyazungumza na ili kila upande uweze kujiridhisha.
Aidha alisema mradi wa nyumba za Mbweni umefanyiwa utafiti na hakuna fedha za wananchi zilizopotezwa hadi.
Alisema serikali itaendelea na jitihada ya kukusanya mapato ili Zanzibar iweze kujiendesha wenyewe badala ya kutegemea wahisani
Alisema katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali ilikadiria kukusanya mapato kutokana na vyanzo vya ndani shilingi bilioni 675.8 sawa na asilimia 21.8 ya pato la taifa.
Alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 627 zilipangwa kukusanywa kutokana na makusanyo ya vyanzo vya kodi na shilingi bilioni 48.8 kutokana na vyanzo visivyo vya kodi.

Zanzibarleo.

Comments