Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji
Mambosasa
amesema kwamba wameweka vizuizi kila sehemu kuhakikisha hakuna mtu
anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika
kwenye tukio la kumteka ni raia wawili wa kigeni.
Amesema hadi sasa watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam.

Mpekuzi.
Comments