Benki
ya Dunia imepunguza matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa eneo la Afrika,
chini ya jangwa la Sahara mwaka 2018 hadi asilimia 2.7 badala ya utabiri
wa awali wa asilimia 3.1.
Kwa
kiasi kikubwa hali hiyo inatokana na ukuaji wa pole pole wa uchumi
katika bara hilo, kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo juzi Jumatano.
Eneo
hilo, ambalo lilikuwa na ukuaji wa viwango vya wastani vya uchumi miaka
kadhaa kuelekea mwaka 2015, ilipata hasara kubwa katika kasi ya ukuaji
wake baada ya bei za bidhaa kushuka mwaka 2015 – 2016.
Mwezi
Aprili, Benki ya Dunia ilibashiri kwamba ukuaji huenda ungekuwa kwa
kasi zaidi mwaka 2018, ukuaji wa wastani ukiwa katika kiwango cha
asilimia 3.1, ikiwa ni juu kutoka ukuaji wa asilimia 2.3 mwaka 2017.
“Kasi
ya ukuaji wa pole pole barani Afrika chini ya jangwa la Sahara,
unaelezewa kuwa unatokana na upanuzi usiotabirika wa kiuchumi katika
mataifa matatu yenye uchumi mzuri ya Nigeria, Angola na Afrika Kusini,”
taarifa ya benki imesema.
Kushuka
kwa uzalishaji mafuta nchini Angola na Nigeria kumesababisha kupanda
kwa bei za mafuta na nchini Afrika Kusini, ukuaji dhaifu wa matumizi ya
majumbani kumetokana na kupungua kwa shughuli za kilimo, taarifa ya
Benki ya Dunia imesema.
Nchi
zingine katika bara hilo zimekuwa na ukuaji usiotetereka mwaka 2018,
zikiwamo zile ambazo hazitegemei bidhaa, kama vile Ivory Coast, Kenya na
Rwanda, benki imeongezeka kusema.
Albert
Zeufack, mchumi mkuu kwa Afrika katika Benki ya Dunia, amezisihi
serikali katika eneo hilo kuacha kutumia fedha vibaya na badala yake
kuboresha uzalishaji ili kusaidia katika harakati za kufufua uchumi.
Madeni
makubwa ya umma katika baadhi ya nchi kwenye bara hilo, ukichanganya na
sarafu dhaifu na kupanda kwa viwango vya riba, huenda kukahatarisha
uwezo wa kulipa madeni yao, Benki ya Dunia imeonya.
“Watunga
sera katika eneo hilo lazima wajiweke sawa kukabiliana na hatari mpya
ambazo zinajitokeza kutokana na mabadiliko katika mtiririko wa mitaji na
madeni,” Zuefack anaesema.
Mpekuzi.
Comments