RC Makonda Aagiza Kukamatwa Kwa Vigogo Waliohujumu Soko La Kariakoo Na Kusababisha Hasara ya Bilioni 1.3
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa
waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia
serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.
Vigogo
walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya
utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na
biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja.
RC
Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za
wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa
watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini
uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha Nyuma wafanyabiashara.
“Hatuwezi
kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha
Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo
600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo
analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani” Alisema RC
Makonda.
Aidha
RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina
ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru
ifanywe na uongozi wa soko.
Pamoja
na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la kariakoo kurejeshwa kwenye
hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela Kama ilivyo sasa ambapo
linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza
bidhaa za jumla.
Miongoni
mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya
viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru,
mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya
vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi
kuzifanyia kazi.
mPEKUZI.
Comments