Rais Magufuli Apokea hati za utambulisho wa mabalozi 5.....Atoa Neno Ujenzi wa Stiegler's Gorge na kiwanda cha kuchakata gesi.
Rais
John Magufuli leo Oktoba 4, 2018 amepokea hati za utambulisho wa
mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, mabalozi hao ni kutoka
Palestina, Kuwait, Norway, Ubelgiji na Sweden.
Rais
Magufuli amepokea hati hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.Miongoni mwa
watu waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Mahiga na viongozi wengine.
Mabalozi
hao walipowasili Ikulu kila mmoja kwa wakati wake kwa msafara maalum wa
askari polisi wenye pikipiki, walipigiwa wimbo wa taifa kabla ya
kuendelea na hatua ya kukabidhi hati.
Mara
baada ya kila mmoja kuwasilisha hati zao, wamefanya mazungumzo na Rais
Magufuli kwa muda mfupi kisha kutoka na kupigiwa wimbo wa Taifa huku
gari aliloingia nalo, linapandishwa bendera ya nchi yake wakati
anaondoka.
Balozi
wa Norway kabla ya kuja nchini alifanya kazi nchini Afghanistan kwa
miaka mitano huku wa Kuwait alifanya kazi Romania na Marekani
Katika utambulisho huo, balozi wa Palestina alimsalimia Rais Magufuli kwa lugha ya Kiswahili akichanganya na Kiarabu.
“...Asalamu aleykum, nimefurahi kukutana na Rais wa Tanzania...” alisikika akisema
Mara
baada ya mabalozi hao kumaliza kupokea hati, Balozi Mahiga amesema Rais
Magufuli amemsisitiza Balozi wa Norway kuikumbusha nchi yake kumaliza
mapema mazungumzo kuhusu kampuni ya State oil na Sheli.
Amesema
mazungumzo hayo yanayoendelea kwa kusuasua, lengo lake ni kampuni hizo
mbili kushirikiana kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ili iuzwe nje ya
nchi.
Balozi
Mahiga amesema eneo la kujenga kiwanda limeshapatikana na gesi pia ipo,
hivyo mazungumzo hayo yakikamilika kila kitu kitakwenda kama
kilivyopangwa.
Kuhusu
ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji
(Stiegler's Gorge), Rais Magufuli amemwambia balozi wa Sweden mbuga ya
Selous haina manufaa kwa Tanzania bali kwa ulimwengu mzima.
“Rais
amemueleza ni asilimia 1.3 ya eneo la mbuga ya Selous ndiyo limetumika
kwenye mradi huo, ambao ni muhimu kwa sababu ukikamilika utawahakikishia
Watanzania nishati ya umeme, tofauti na hapo wataendelea kukata miti na
hata hiyo mbuga haitakuwapo tena, ”amesema Balozi Mahiga.
Amesema
Rais Magufuli amemweleza Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imetenga
asilimia 32.5 ya ardhi yake kwa ajili ya hifadhi ya misitu na wanyama.
Mpekuzi.
Comments