Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe ya uchaguzi katika majimbo
ya Simanjiro na Serengeti pamoja na kata 21 za Tanzania Bara ambapo
unatarajiwa kufanyika Desemba 2, 2018 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage ambapo
amesema kuwa fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 28
Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.
“Uteuzi
wa Wagombea utafanyika tarehe 03 Novemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi
zitafanyika kuanzia tarehe 04 Novemba hadi tarehe 01 Desemba mwaka huu
na siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 2 Desemba, mwaka huu,” amesema
Jaji Kaijage.
Amesema
kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu tume uwepo wa nafasi za wazi za Ubunge
katika Majimbo mawili (2), Jimbo la Serengeti lililopo Halmashauri ya
Serengeti Mkoani Mara na Jimbo la Simanjiro lililopo Halmashauri ya
Simanjiro Mkoani Manyara.
Aidha,
Kaijage amesema kuwa barua hiyo imepokelewa kufuatia Wabunge wa Majimbo
hayo ambao ni Marwa Ryoba Chacha, na James Ole Millya kujiuzulu na
kutoka kwenye vyama vyao vya awali.
Amesema
Tume pia imepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali
za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1)
cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume uwepo wa
nafasi wazi za Madiwani katika Kata 21 za Tanzania Bara. ambapo nafasi
hizo wazi zimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kujiuzulu.
Hata
hivyo, amezitaja kata zenye uchaguzi na halmashauri zake kwenye mabano
ambapo ni pamoja na Ilboru, Mlanfarini na Oldonyosambu (Wilaya ya
Arusha), Engutoto na Olasiti (Manispaa ya Arusha), Hazina (Manispaa ya
Dodoma), Chinugulu (Wilaya ya Chamwino), Kasharu, Nyakimbili, Kishongo
(Wilaya ya Bukoba), Chonyonyo, Ihanda (Wilaya ya Karagwe).
Nyingine
ni pamoja na Muhindawa, Mnanila (Wilaya ya Buhigwe), Mnerongongo
(Wilaya ya Nachingwea) Ngarenairobi (Wilaya ya Siha), Kyanyari (Wilaya
ya Butiama), Namilembe (Wilaya ya Ukerewe), Lukanga, Beta (Wilaya ya
Mkuranga) na Chikola (Wilaya ya Manyoni).
Mpekuzi.
Comments