Mwanafunzi
wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Jumbi, Sabra Ussi Khamis
amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtu
anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili.
Tukio
la kuuawa kwa binti huyo limetokea jana Oktoba 2, 2018 majira ya saa
mbili usiku wakati Sabra alipokua akiuza duka nyumbani kwao na ghafla
alitokea kijana huyo anayesadikiwa kuwa mgonjwa wa akili Hafidh Mkubwa
Suleiman (21) na kumchoma na kitu tumboni.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka amesema ni
kweli tukio hilo limetokea na wanaendelea na uchunguzi kubaini taarifa
zaidi.
Mpekuzi.
Comments