Jeshi
la Polisi mashariki mwa mji wa Eldoret, kaunti ya Uasin-Gishu magharibi
mwa Kenya imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 28, Andrew Kimutai,
akituhumiwa kumuua baba yake, Joseph Marindany .
Akithibitisha
tukio hilo OCPD wa Eldoret Mashariki Bw Richard Omanga, amesema kuwa
Andrew anatuhumiwa kumuua baba yake kwa kumkata kichwa kwa kutumia
shoka, baada ya kukataa kumpa kondoo wa familia ili alipe mahari
kukomboa mtoto wake wa kiume aliyempata nje ya ndoa.
“Marehemu
alikataa kumpa mwanawe kondoo kwa sababu hakujua alikuwa amezaa mtoto
nje ya ndoa kama alivyodai. Mshukiwa alikasirishwa na msimamo wa baba
yake ndipo alimvamia baba yake akiwa chumbani mwendo wa saa moja,
akamkatakata kwa shoka,” alisema OCPD Omanga.
Mtuhumiwa
huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Naiberi akisubiri
kufunguliwa mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika.
Comments