Mkongo
wa Taifa wa Mawasiliano umeongeza makusanyo ya mapato ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maeneo ya mipakani mwa Tanzania
na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi na DRC Congo
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kukagua Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano kwenye kituo cha mpakani cha Mtukula ambacho kinawezesha
usafirishaji wa taarifa na data za wateja na bidhaa kutoka Tanzania
kwenda nchi jirani ya Uganda.
Nditiye
amesema kuwa, “maeneo ya mipakani ndi lango la kuongeza mapato na
kukuza uchumi wan chi yetu, niwatake muendelee na kasi hii ya ukusanyaji
wa mapato ya Serikali kwa kutumia Kituo cha Pamoja cha Huduma ambapo
tayari kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka wa fedha wa
2018/2019, mwezi Julai hadi Septemba, 2018 mapato yameongezeka zaidi ya
asilimia 100 kwa mwezi na kufikia asilimia 150”.
Naye
Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Huduma cha Pamoja cha Mtukula,
Bwana Mohammed Shamte amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019,
malengo yao ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 15.9 kwa mwaka
ambapo tayari imeonekana kiwango hicho kitafikiwa kwa kuwa tayari kwa
mwezi wanakusanya shilingi bilioni 1.3 ambazo ni wastani wa asilimia 110
hadi 150 ya makusanyo kwa mwezi ambayo yanavuka malengo.
“Baada
ya Serikali kuweka Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, umeongeza spidi na
uhakika wa kusafirisha taarifa na data tofauti na hapo awali tulipokuwa
tunatumia satelaiti, hivyo Mkongo umewezesha ongezeko la mapato”,
amesema Shamte.
Nditiye
ameongeza kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umebadilisha sekta ya
mawasiliano nchini na kwenye nchi za jirani zilizounganishwa na Mkongo
huo za Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na DRC Congo ambapo wanafurahia
huduma za mawasiliano.
“Mkongo
wa Taifa wa Mawasiliano lazima ulindwe, ni kama reli au barabara, na
mawasiliano ni uchumi na maendeleo ambapo unaingiza mapato kwa Serikali
yetu,” amesema Nditiye
Pia,
amewataka wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL
Corporation) waendelee kuutunza na kuendesha Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano kwa kuwa ni watu sahihi, wana utaalamu na ujuzi wa kutosha
kufanya kazi na Serikali imewaamini na kuwapa jukumu hilo kwa kuwa
mawasiliano ni uchumi na ni usalama hivyo ukicheza na mawasiliano nchi
inasambaratika.
Wakiwasilisha
changamoto za mawasiliano kwa Nditiye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Misenyi Bi. Thabitha Solomoni amesema kuwa wakati mwingine
mtandao unakwenda taratibu au kukosekana hivyo kuathiri usafirishaji wa
taarifa na data za watumishi kwa Serikali wa malipo na masuala ya
watumishi
Naye
Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera Bi. Irene Shayo amejibu changamoto hio
kwa kusema kuwa inategemea aina ya kifurushi ambacho Halmashauri husika
imenunua na wanachotumia.
Ametoa
rai kwa Halamshauri kutumia wataalamu wao kufahamu uwezo wa mtandao wa
intaneti wanaotumia ili uweze kuendana na mahitaji na ukubwa wa taarifa
au data wanazotuma au kupokea, hivyo Ofisi za Serikali zizingatie ubora
wa huduma kuendana na mahitaji yao na TTCL ina ofisi zake nchi nzima,
wako tayari kuwahudumia.
Nditiye
amepokea changamoto hiyo kuhusu spidi ya intaneti kwenye ofisi zao na
amewataka wataalamu wa TEHAMA kupeleka mahitaji sahihi ya mtandao wa
intaneti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zao na TTCL wako tayari kushauri
ili mahitaji yanayotakiwa yaweze kutolewa na TTCL kuendana na mahitaji
stahiki
Naye
Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bwana
Mulembwa Munaku amewataka maafisa TEHAMA wote kufungia mitandao ya
kijamii muda wa saa za kazi ili mtandao wa intaneti uweze kutumika
vizuri kwa matumiz ya Serikali
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemweleza Nditiye
kuwa bado hakuna mawasiliano ya kuridhisha kwenye maeneo mbali mbali ya
mkoa huo licha ya kwamba makampuni yote ya mawasiliano yapo ila bado
kuna changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika kwenye mkoa huo
Akitoa
ufafanuzi kuhusu changamoto hiyo, Nditiye amesema kuwa tayari Serikali
imechukua hatua kuhusu jambo hilo kwa kuongeza minara ya mawasiliano
kwenye maeneo ya mipakani ambapo mawasiliano ni hafifu kwa kuwaelekeza
wataalamu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kufika kwenye maeneo hayo,
kufanya tathmini na kupeleka mawasiliano kwa kuwa hadi sasa watanzania
wanapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 94 isipokuwa maeneo
machache.
Pia
ameipa TTCL mwezi mmoja kuhakikisha vocha na laini za TTCL zinapatikana
nchi nzima ili kuwawezesha watanzania kuwasiliana kwa kuwa mawasiliano
ni uchumi na ni usalama
Nditiye
amefanya ziara hiyo ya kukagua miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano kwenye vituo vya mpakani vya Kabanga, Rusumo Mtukula na
Biharamulo
mPEKUZI.
Comments