Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Khamis Abdulrahman Msham, alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jana.
Alisema, mfuko wa bei za chakula na bidhaa zisizokuwa na vileo
zilishuka kwa asilimia 0.1 kwa mwezi Septemba kutoka 1.9 kwa mwezi
Agosti 2018.
Alisema, faharisi za bei kiujumla ziliongezeka hadi 107.9 mwezi Septemba 2018 ikilinganishwa na 104.3 mwezi Agosti, 2017.
Aidha, alisema, kiwango cha mfumko wa bei cha mwaka kwa vyakula
kilikuwa asilimia 0.0 kwa mwaka uliomalizikia Septemba 2018
ikilinganishwa na asilimia 2.0 mwaka ulioishia Agosti, 2018.
Alisema, faharisi za bei za vyakula zilibakia 105.6 mwezi Septemba 2018 kama zilivyokuwa mwezi Septemba 2017.
Lakini, faharisi za bei kwa bidhaa zisizokuwa za vyakula ziliongezeka
hadi 109.7 mwezi Septemba, 2018 ikilinganishwa na 103.3 mwezi Septemba
2017.
Bidhaa zilizochangia kushuka kwa kiwango cha mfumko wa bei kwa mwaka
zilikuwa unga wa sembe (12.8%), ndizi za mtukwe (11.8%) na sukari (5.2).
Alisema, kwa upande wa mfumko wa bei wa mwezi Septemba, ulishuka kwa asilimia 1.3 ikilinganishwa na 1.0 mwezi Agosti 2018.
Alisema, mfumko wa mwezi kwa bei za vyakula na bidhaa zisizo na
vilevi kwa mwaka ulioishia Septemba 2018, ulikuwa asilimia 2.4
ikilinganishwa na asilimia hadi 1.7 kwa mwaka uliomalizikia Agosti,
2018.
Kupungua kwa kiwango cha mwezi cha mfumuko wa bei kulichangiwa na bei
ya vitu kama mchele wa mapembe (-0.4%), Mbeya (-1.0%), samaki (-5.6%),
sukari (-1.0%), dizeli (-0.8 %), petroli (-0.4%) na mafuta ya taa
(-1.3%).
Mkuu wa Takwimu za Uchumi, Abdulrauf Ramadhan Abeid, alisema, kwa
ujumla katika nchi tatu za Afrika Mashariki mfumko bado upo chini ya
tarakimu moja na hivyo kwenda vizuri.
Alisema, mfumko wa bei uliongezeka kwa asilimia 5.7 ikilinganishwa
na asilimia 4.0 wakati Uganda ulishuka kutoka asilimia 3.8 na
kufikia 3.7.
Zanzibarleo.
Comments