Aliyekuwa
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul amejibu madai ya baadhi ya makada
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wanaomshutumu kuandikiwa
barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kutokana na barua hiyo kuwa na
kasoro na kufanana na barua zingine za wabunge waliojiuzulu kabla yake.
Gekul
amesema kuwa wanadamu wakiamua kukutaftia kosa hawawezi kukosa cha
kuongea hivyo amewataka Chadema wahangaike kujibu hoja zake na si kuanza
kuangalia vitu binafsi.
“Wanadamu
wakiamua kutafuta makosa kwako hawayakosi, utakuwa mtu wa ajabu
unayeangalia zaidi maandishi badala ya ujumbe wa barua, uandishi wa
barua mimi siangalii, kwangu sikuona kama ni hoja.”amesema Gekul
Amesema
kuwa makosa ya kiuandishi hutokea popote, hivyo kukosewa kuandikwa kwa
barua yake ya kujiuzulu sio tatizo lakini chamsingi ni ujumbe umefika
sehemu husika na wala sio lugha iliyotumika, hivyo amewataka wahangaike
na kujibu hoja zake.
Hivi
karibuni katika mtandao wa Twitter afisa habari wa CHADEMA, Tumaini
Makene alikosoa uandishi wa barua za wabunge waliojiuzulu kwa madai kuwa
ni za aina moja.
Pauline
Gekul ametimiza idadi ya wabunge 8 kutoka vyama vya upinzani
waliotangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai mbalimbali
ikiwemo kumuunga mkono Rais Magufuli.
Mpekuzi.
Comments