Alisema hayo wakati akizungumza na mawakala wa kazi katika ukumbi, Mwanakwerekwe mjini Unguja.
Alisema, mawakala wanafanya kazi kinyume na taratibu zilizowekwa na wanawatoza pesa wananchi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi kwa misingi ya kwamba hakuna kitu cha bure, jambo ambalo ni kosa kisheria.
“Tunapokea malalamiko kutoka kwa wananchi, kwamba mawakala wa kazi wanafanya haya kwa makusudi, tunawaomba wafuate taratibu”, alisema.
Aidha alisema, sheria za kimataifa na ndani, zinakataza kuwatoza pesa wananchi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi.
“Lakini inawezekana wengi wa mawakala wetu hawafahamu taratibu ambazo tunatakiwa tuzitumie katika suala zima la kuwasafirisha wafanyakazi”, alisema.
Aidha alisema, lengo la kukutana na mawakala hao ni kukumbushana kuwa, wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi.
Zanzibarleo.
Comments