Masheikh, maimamu wahamasishwa uchangiaji damu.

WAZIRI wa Afya, Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa viongozi wa dini wananafasi kubwa katika jamii katika kuhamasishaji wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo suala la uchangiaji wa damu salama.
Alisema iwapo maimamu wa misikiti watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha waumuni kuchangia damu tatizo la damu litaondoka katika hospitali zote hapa nchini.
Waziri huyo alieleza hayo huko Benki ya damu salama Sebleni katika mkutano wa uhamasishaji wa uchangiaji damu kwa maimamu wa misikiti mbali mbali ya Unguja.
Aidha alisema uchangiaji damu ni suala lenye umuhimu wa kipekee kwani kila mmoja anaweza akahitaji damu wakati wowote hivyo amewataka wananchi kulipa kipa umbele na kuondokana na upungufu katika Benki ya damu na hospitali.
Alifahamisha kuwa wizara ya Afya kupitia mpango wa damu salama watafanya kila jitihada ya kuwepo vituo kwa kila wilaya vya kukusanyia damu ili kuweza kukabilina upungufu wa hali ya upatikanaji damu.
Kwa upande wake ofisa uhamasishaji wa Benki ya damu salama Bakari Magarawa alisema kumekuwa na mashirikiano mazuri na taasisi ya kidini pamoja na vikosi vya serikali na jamii ambapo wanasadia upatikanaji wa damu kwa kiasi kikubwa.
Zanzibarleo.

Comments