Akizungumza
katika eneo la maonyesho Afisa mdhamini wizara ya ardhi nyumba maji na nishati
Zanzibar Juma Bakari Alawi amesema kiujumla wananchi wamehamasika kuweza
kushiriki maonyesho hayo kikamilifu.
Amesema
hiiyote nikutokana na waliowengi kuweza kuitikia wito wa serekali wakushirikia
kikamilifu ili kujifunza mambo mbali mbali yanayopatikana katika maonyesho hayo
ya siku ya chakula Duniani nao waweze kuyatumia baada ya kukamilika kwake.
Aidha
amewataka wananchi na wajasiriamali kwaujumla kujifunza mbinu mbali mbali za
kilimo ambazo zitawasaidia wao kuweza kuendana na kilimo cha kisasa ambacho
kitaweza kutoa tatizo la njaa hapa nchi.
Omar
Rashid Omar Afisa mkuu Idara ya Mipango na Utumishi Kutoka Wizara ya Kilimo
Maliasili Mifugo na Uvuvi Pemba amesema wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa
wingi kujionea maonyesho hayo nakuweza kutoa michango yao ambayo yatawasaidia
kuweza kuondoa changamoto ambazo zimeonekanwa.
Amefahanisha
kuwa wananchi watambue maonyesho hayo sio yawizara ya Kilimo pekee baliniyakila
mwananchi anayo fursa yakuweza kushiriki kikamilifu kwani yanaweza kuwaongezea
uwelewa juu ya mazao yakilimo nayale yakibiashara.
Kwaupande
wake Afisa masoko kutoka Benk ya Watu wa Zanzibar Asia Khamis Shaaban maesema
maonyesho hayo yameweza kuwapa faraja kwao na kwanawananchi kwani walio wengi
walikua hawajui matumizi sahihi ya kibank nao kuweza kutoa elimu hiyo
kwalioweza kuhudhuria katika kibanda chao.
Nao
baadhi ya wananchi waliopana nafasi yakutoa maoni yao wameitaka srekali
kuyafanya maonesho hayo kuwa endelevu kila mwaka kwani yanatoa hamasa na
mafunzo ambayo nayawasaidia kujikomboa kimaisha.
Kaulimbiu
ya maonyesho hayo ni juhudi zetu ndio hatma zetu dunia bila njaa inawezekana
ifikapo mwaka 2030.
Comments