Manispaa yawataka wananchi kutupa taka kwenye makontena.

JAMII imetakiwa kutupa taka zao katika makontena  yaliyowekwa na Baraza la Manispaa, ili kuepusha uchafunzi wa mazingira hususan katika kipindi hichi cha mvua za vuli zinazoendelea kunyesha.
Wito huo, umetolewa na Mkuu wa Huduma za Jamii na Mazingira, Rajab Salum Rajab, kutoka Baraza la Manispaa Mjini, wakati alipokuwa akizungumza namtandao huu, kufuatia kituo cha Kwabitiamrani kutupwa taka chini pamoja na uvamizi unaofanywa kwa wenye magari kutupa taka maeneo hayo nyakati za usiku.
Hivyo, alisema ni vyema wananchi wakahakikisha wanashughulikia matatizo ambayo yanaanza kujitokeza kabla kusikia baraza hilo , kwani kufanya hivyo kituo hicho kitakuwa kizuri na taka zitaweza kumwagwa katika utaratibu uliokusudiwa.
Zanzibarleo.

Comments