Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepokea hati ya kifo ya
mshtakiwa wa tatu Benjamin Mwakatumbula aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya
uhujumu uchumi na kusababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 1.16,
pamoja na wenzake akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
(NIDA) wa zamani, Dickson Maimu.
Mwakatumbula
wakati wa uhai wake alikuwa Kaimu Mhasibu Mkuu wa Nida, hati ya kifo
chake iliwasilishwa na upande wa utetezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa jana.
Wakili Serikali Imani Mitumizizi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na ilipangwa kwa ajili ya kutajwa.
Hata
hivyo, mshtakiwa Maimu aliwakabidhi Wakili wa utetezi Faisal Ali
bahasha ya kaki na ilipofunguliwa ilikuwa na hati ya kifo na kuikabidhi
mahakama.
Hakimu
Mashauri alisema mahakama imepokea hati ya kifo cha Mwakatumbula na
mwenendo wa kesi dhidi yake umefutwa.Alisema kesi hiyo itatajwa tena
Novemba 15,mwaka huu dhamana ya washtakiwa inaendelea.
Mbali
ya Maimu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa
NIDA, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji,
George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Katika
kesi ya msingi, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka
vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na
kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. 1,169,352,931.
Mpekuzi.
Comments