Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na
wakili wa upande wa mlalamikiwa namba mbili, mfanyabiashara wa mabasi
ya Batco, Baya Malagi, kwenye kesi ya mauziano ya Hoteli ya Tai Five
ya Mwanza.
Kesi
hiyo ya madai ya ardhi namba 46 ya mwaka 2017 ilifunguliwa na
aliyekuwa mmiliki wa hoteli hiyo iliopo Nyamanoro jijini hapa,
Christopher Tarimo, mwaka 2017 katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Issa Maige alitoa hukumu hiyo jana katika kesi ya msingi.
Alisema
mapingamizi ya sheria yaliyowekwa na wakili upande wa mlalamikiwa
namba mbili, mfanyabiashara Kusaga Malagi hayana msingi.
Mapingamizi
hayo mawili yalikuwa ni kufanana kwa shauri lililokuwapo mahakamani
hapo mwaka 2011 na pingamizi jingine lililowekwa, kuwa ni usumbufu kwa
mahakama kusikiliza kesi kwa mara nyingine.
Upande
wa mujibu maombi namba moja ambayo ni Benki ya CRDB uliwakilishwa na
Wakili Galati Silwane, huku upande wa mlalamikiwa namba mbili
ukiwakilishwa na Wakili Emmanuel Anthony.
Upande
wa mlalamikaji Christopher Tarimo uliwakilishwa na mawakili Julius
Mushumbusi na Mwita Emmanuel kutoka Kampuni ya Wanasheria ya Kailu Law
Chembers.
Baada
ya kusikilizwa pande zote mbili kuhusu hoja hizo, Jaji Maige alisema
mahakama imeona kulikuwa na utata mkubwa katika mauziano ya Hoteli ya
Tai Five yaliyofanyika kati ya mlalamikiwa namba moja na mbili.
Jaji
alisema mauziano hayo pia yalighubikwa na mambo ya sintofahamu na
kwamba mauziano hayo yalifanyika bila kukazia hukumu ya kesi namba 4 ya
2011.
Pia
alisema mauziano ya wajibu maombi yanaonekana kama yalifanyika baina ya
waleta maombi ambao ni Tai Five Ltd na Christopher Tarimo na mjibu
maombi namba moja ambayo ni The Mogeji Instruments.
Waandishi
walipomtaka wakili wa upande mlalamikaji, Mwita Emmanuel kuzungumzia
uamuzi huo alidai suala hilo wanaiachia mahakama yenye mamlaka ya
kutenda haki.
Mpekuzi.
Comments