Mahakama
ya Hakimu Mkazi Iringa imepanga kusoma hukumu ya kesi inayomkabili
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania, Abdul Nondo
Novemba 5.
Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kusema uongo ambayo anadaiwa kuyatenda Machi 7, mwaka huu.
Akitaja
tarehe ya hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Iringa, Liad
Chamshama alisema jana Jumanne ilikuwa ni siku ya kuwasilisha hoja za
mwisho za upande wa utetezi na upande Jamuhuri.
Upande
wa mshtakiwa uliwakilishwa na Wakili Baruti baada ya mawakili Jebra
Kambole na Chance Luwoga kuwa nje ya mkoa ambapo wakili huyo ameridhia
kusomwa kwa hukumu ya mteja wao Novemba 5, mwaka huu.
Awali
Abdul Nondo alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashtaka mawili
ambapo shitaka la kwanza lilikuwa ni kusema uwongo kwa njia ya mtandao
wa kijamii wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Shitaka
la pili linalomkabili Abdul Nondo ni la kusema uongo kwa mtumishi wa
umma ambaye ni askari wa Kituo cha Polisi Mafinga kuwa alitekwa na watu
wasiofahamika Dar es salam na kutelekezwa Kiwanda cha Pareto Mafinga.
Pande zote mbili zimefunga kuleta ushahidi na mahakama imepanga tarehe hiyo kuwa siku itakayosomwa hukumu hiyo.
Mpekuzi.
Comments