Uchaguzi
wa Naibu Meya wa jiji la Dar es salaam jana ulilazimika kuahirishwa
kutokana na wajumbe wa mkutano huo kutoafikiana kwa baadhi ya vipengele,
ikiwemo kutokukubaliwa kwa hati ya mgombea wa nafasi hiyo aliyetokea
(UKAWA) kupitia Chama Cha Wananchi CUF.
Katika
mkutano huo ilishuhudiwa baadhi ya wajumbe akiwemo Mbunge wa Kawe,
Halima Mdee na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea wakiingia kwenye malumbano
ya maneno na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Riama juu ya hati ya mgombea
huyo.
"Tunaomba
hoja iliyotolewa na mjumbe Ndugulile aipokee Mkurugenzi na aseme
ameikubali ili twende mbele, mheshimiwa ndugulile tumuulize Mkurugenzi
amekubali kuja na utaratibu mpya kwenye kikao kijacho", alisema Kubenea.
"Kwanini
unaingilia majukumu yangu, huyu naye ni (Meya wa jiji) ana maslahi
hawezi kutoa miongozo, mimi nina wanasheria hapa, maafisa utumishi ili
kusimamia uchaguzi na miongozo mimi ndo natoa", alisema Sipora wakati
akizungumza kwa sauti kwenye kikao hicho.
"Nimshukuru
Mheshimiwa Ndugulile, kwa kuwa tumekubaliana kuhairisha kikao, naomba
UKAWA kupitia chama cha wananchi CUF kipate haki yake ya kupata mgombea
wake, tunaomba kikao kinachokuja ajenda moja wapo iwe ni uchaguzi",
alisema Mdee kwa kumalizia.
Awali
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto, Dkt
Faustine Ndugulile alitoa ushauri wa kuhairishwa kwa ajenda ya uchaguzi
kwenye kikao hicho, hoja ambayo ilikuja kukubaliwa mwishoni mwa kikao.
"Kikao
chetu kimedumu kwa zaidi ya saa 4 kitu ambacho nakiona hapa, mjadala
huu hautafika mwisho, naomba tuhairishe ajenda ya uchaguzi mpaka siku
nyingine".
MPEKUZI.
Comments