Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Faraji Mnyepe amesema watendaji katika wizara hiyo wamezoea kufanya kazi
kwa mazoea kuwa kituo cha kufanyia kazi ni nje ya nchi.
Dk. Mnyepe amesema hayo leo Jumatano Oktoba 3, Ikulu jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo.
“Nikutoe
hofu Mheshimiwa Rais, nakwenda kufanya kazi sina wasiwasi na idhini
yako uliyonipa nikafanye kazi. Nilisikia ulipomuapisha Naibu Waziri
(Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Damas Ndumbaro) ulisema wazi wizara hiyo haifuraishi.
“Ulitoa
sababu na sababu zile ni za kweli zote. Matatizo ya wizara yako mengi
lakini katika salamu zangu hizi naomba niyakweke katika sehemu mbili, ya
kwanza barua kwa nini hazijibiwi.
“Mentality
(dhana) au culture (utamaduni) ni kwamba ukishaajiriwa katika wizara
ile kituo chako cha kazi ni nje ya nchi, kwa hiyo mtu ukishateuliwa
ukirudishwa unarudishwa ili utafutiwe kituo kingine cha kazi, hiyo ndiyo
mentality.
“Kuna
makundi katika wizara ile kama ulivyoanisha siku ile, mengi sana…
Mheshimiwa rais naenda kuishi katika kiapo changu,” amesema Dk. Mnyepe.
Mpekuzi.
Comments