Waziri
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemuagiza Inspekta Jenerali wa
Polisi, Simon Sirro, kupunguza vituo vya ukaguzi wa magari visivyo na
lazima ambavyo vimeonekana kutumiwa vibaya na askari wa usalama
barabarani wasio waadilifu.
Lugola
ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 3, wakati akizungumza na waandishi
wa habari katika ziara yake Mjini Mbeya akitokea mkoani Rukwa.
Amesema
vituo hivyo ambavyo vilivyowekwa baada ya kila hatua 20 kwa lengo la
kudhibiti ajali, vimegeuzwa na kuwa fursa kwa baadhi ya askari.
“Askari
wamekuwa wakiwaumiza wananchi, wanasimamisha magari kila kituo, vituo
vipo kila zaidi ya hatua 20, halafu kazi kubwa ni kuomba na kupokea
rushwa,” amesema Lugola.
Mpekuzi.
Comments