Jong’ombe ichagua CCM kwa maendeleo yenu.

WANANCHI wa jimbo la Jang’ombe wametakiwa kumchagua mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ili kuweza kuendelea kuwapelekea maendeleo katika jimbo hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib aliyasema hayo alipokuwa akimnadi mgombe wa uwakilishi wa jimbo hilo katika uwanja wa Jang’ombe Urusi, wilaya ya Mjini Unguja.

Alisema CCM ndio chama pekee chenye kuleta maendeleo kwani kimekuwa kinaendeleza kuitunza Amani iliyopo, hivyo aliwataka wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo kutokufanya makosa wakati utakapofika.

Alisema historia ya CCM ndani ya Jang’ombe iliongozwa na viongozi waliokuwa na uwezo na upeo uliokuwa mkubwa, hivyo aliwataka wananchi hao kumchagua mgombea kupitia CCM ili kuweza kuendeleza mazuri yaliyofanywa na viongozi waliopita.

Mbali na hayo alimtaka mgombea huyo kuwa karibu na viongozi wenzake katika kutekeleza majukumu ya kazi pamoja na kuendelea kuhubiri Amani iliyopo katika nchi.

Nae Julius Mtatiro, ambae aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa Chama cha CUF kwa muda wa miaka 10, alisema hakuona chama kinachoweza kuwapelekea wananchi maendeleo isipokuwa CCM, hivyo aliwataka wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo, kumchagua mgombea wa CCM ili kuweza kuwafikishia maendeleo.

Sambamba na hayo aliwasisitiza wanaCCM kuwa na imani na CCM kwani Chama hicho kipo kwa lengo la kuwatumikia wananchi na kuweza kutatua changamoto za wananchi Tanzania bara na Zanzibar bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Nae mgombea wa Kiti cha uwakilishi, Ramadhan Hamza Chande, aliahidi kushirikiana na wananchi wote wakiwemo vijana ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika jimbo
hilo.

Sambamba na hayo aliwaahidi wananchi wa urusi endapo wakimpa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo, atatulia tatizo la maji ambalo limekuwa limedumu kwa kipindi kikubwa katika shehia hiyo.

Comments