Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Makame Ali Ussi, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ofsini kwake Maruhubi.
Alisema tani hizo zimepatikana baada ya kikosi hicho kufanya bidii katika uzalishaji kwa lengo la kuimarisha sekta ya kilimo nchini.
Aidha alisema katika kuhakikisha wakulima wanafuata taratibu wameandaa vitabu 2,000 na vipeperushi kwa ajili ya kuhamasisha matumizi bora ya mbegu zilizochaguliwa na wakulima ambazo ni SARO na SUPA BC.
Alisema kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji wa mpunga kupitia mradi wa ERPP.
Akizungumzia suala la ukaguzi alisema zaidi yatani 19000 za mazao mbalimbali yaliotoka nje ya nchi yamekaguliwa katika kipindi cha mwezi Septemba.
Alisema katika ukaguzi huo jumla ya mazao yaliyoingia kutoka Tanzania bara ni 3,126.17 ambapo mazao yaliyokaguliwa kutoka nchini za nje ni tani 13,787.0.
Alisema kuwa mazao yaliyokaguliwa yalisafirishwa kwenda Oman na Dubai kupitia uwanja wa ndege ambayo ni wastani wa tani 1.324.
Zanzibarleo.
Comments