Jiji
la Mbeya linalo ongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
kupitia Mbunge wake, Joseph Mbilinyi maarufu kama “SUGU” limetajwa kuwa
ni jiji la mwisho kwenye ukusanyaji wa mapato katika orodha ya majiji
hapa nchini ikiwemo Dar es salaam, Dodoma, Arusha, Tanga pamoja na
mwanza.
Jiji
lililo ongoza kwenye ukusanyaji wa mapato ni Dodoma ambalo lilitangazwa
na Rais Magufuli mwaka huu, ambapo imekusanya zaidi ya shilingi bilioni
25 ambayo ni sawa na asilimia 130 ya matarajio ya ukusanyaji kodi wa
jiji hilo.
Akizungumza
katika mkutano na wadau wa halmashauri nchini juu ya hali ya ukusanyaji
wa mapato katika halmashauri zao, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo ameilitaja Jiji la
Mbeya lililo chini ya utawala wa CHADEMA limekuwa la mwisho kwa
kukusanya bilioni 7.8 ambayo sawa na asilimia 70 ya matarajio.
“Naomba
Wakuu wa Mikoa wanifuatilie ili wakafanyie kazi kwenye majiji yao, Jiji
la Dodoma limekuwa la kwanza kati ya majiji sita kwa kukusanya zaidi
shilingi bilioni 25 sawa na asilimia 130, wakati huohuo jiji la Mbeya
limekuwa la mwisho kwa kukusanya bilioni 7.8 na makadiro yake yalikuwa
bilioni 11”, amesema Waziri Jaffo.
“Kwa
upande wa Manispaa, Iringa mjini ndiyo imeibuka kinara ikifuatiwa na
Manispaa ya Temeke kwenye ukusanyaji wa mapato.” Ameongeza.
Mpekuzi.
Comments