Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema Makosa
mbalimbali ambayo yanafanywa na wanaoendesha vyombo vya moto barabarani
yamesababisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupata
zaidi ya Sh.Bilioni 2.74.
Mambosasa aliyasema hayo jana
ambapo alifafanua kuwa jeshi hilo linaendelea na operesheni ya
kuwasaka madereva wa magari na watumiaji wa vyombo vya moto ambao
hawazingatii sheria ya usalama barabarani.
Alisema
katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari madogo,maroli,
pikipiki na daladala ambapo wahusika wametozwa faini ambapo zaidi ya
Sh.Bilioni 2.74 zimepatikana.
Kamanda
Mambosasa amewawataka watu ambao wametozwa faini za barabani kulipa kwa
wakati kwani kuna tabia ya kulimbikiza deni na wataendelea kuwasaka
wadaiwa wote na iwapo watashindwa gari litachukuliwa na kuwekwa Polisi.
Mpekuzi.
Comments