Baada
ya kumsaka kwa muda mrefu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) imemkamata mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba,
Zacharia Hanspoppe.
Takukuru
imemkamata Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na
kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hanspoppe
alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.
Akizungumzia
kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu, naibu mkurugenzi mkuu wa
Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema, “Ni kweli amekamatwa,
alikamatiwa uwanja wa ndege mara tu alipowasili.”
Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.
“Na
vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata.
Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani kesho (leo).”
Pamoja
na Hanspoppe mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Franklin
Lauwo ambaye naibu mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema kuwa
amekwishawasiliana nao na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya
kurejea nchini akitokea Pakistan.
Mpekuzi.
Comments