Akufunga maonyesho ya siku ya chakula duniani huko
chamanangwe Mkoa wa Kasakazini Pemba amesema Tanzania imepata fursa kubwa
yakupeleka muhogo nchini china fursa ambayo nchi nyingi hawakuipata.
Ameeleza kuwa nimuda sasa kwa wakulima wa muhogo
kuweza kulishughulikia zao hilo ili liweze kuwakomboa na halingumu za
kinmaisha.
Katika hatua nyengine Balozi Seif amewataka vijana
kuachana na tabia ya kusubiri kuajiriwa na serekali na badalayake kuitumia
sekta ya kilimo kama mkombozi wa tatizo la ajira nchini.
Nae naibu waziri wizara ya kilimo maliasili mifugo
na uvuvi Dr. makame Ali Ussi amewashukuru wajasiriamali kwa kushiri kikamilifu
katika kufanikisha maonyesho hayo ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikumbwa.
Maonesho ya siku ya chakula duniani yalifunguliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohd shein Na
kufungwa na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi na
yamegharimu Jumla ya Tsh milioni 140 amapo kaulimbiu ya maonyesho hayo ni
Juhudi zetu Ndio Hazina Yetu Dunia bila njaa inawezekana ifikapo mwaka 2030.
Comments