Ayoub ateua sheha Chuini.

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amemuapisha Sheha wa shehia Urusi, Yussuf Juma Mtumwa, kushika nafasi hiyo, kufuatia aliekuwa sheha wa shehia hiyo, kufariki.
Hafla hiyo ilifanyika ofisini kwake Vuga ikiwa ni kutekeleza matakwa ya sheria ya namba 8 ya tawala za mikoa iliyompa mamlaka ya kuteua masheha katika mkoa wa mjini magharibi.
Akizungumza baada ya kumlisha kiapo sheha huyo, Ayoub, alimtaka kufanya kazi zake kwa mujibu wa shehia na kuwa karibu na wananchi kwa kuwapatia huduma zinazostahiki kwa wakati.
Alisema, kama atakuwa na ushirikiano na wananchi wataweza kufanya kazi zake vizuri.
Pamoja na hayo alimtaka kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria kwa kuwahudumia watu bila upendeleo au ubaguzi.
Pamoja na hayo alimtaka kutumia busara na hekima katika ufanyaji wa kazi zake za kila siku kwani zitasaidia kutatua migogoro inayowakabili wananchi.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib, alimtaka sheha huyo, kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Nae Sheha huyo, alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi waliopo kumpa ushirikiano katika utendaji wa majukumu yake ya kazi.
Wakati huo huo, Ayoub alimtambulisha Kaimu Sheha wa shehia ya Chuini, Mohammed Sheha Kheri.
Kheri anachukua nafasi ya aliekuwa sheha wa shehia hiyo, Juma Mohammed, ambae uteuzi wake ulitenguliwa kutoka na kushiriki katika migogoro ya ardhi.
Zanzibarleo.

Comments