Alichokisema Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza Baada ya Kuapishwa Leo na Rais Magufuli.

Skauti Mkuu wa Chama cha Maskauti Tanzania, Mwantumu Mahiza ameahidi kujenga maadili ya vijana wa kitanzania.

Mahiza ameyaahidi hayo leo tarehe 3 Oktoba 2018 baada ya kuapishwa mbele ya Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Mahiza ameahidi kuieneza skauti katika vyuo vya kati na vyuo vikuu

“Nakushukuru kwa kuniteua kulea vijana wa Tanzania kupitia skauti, wajibu wangu ni mambo mawili, kuhakikisha skauti inaenea katika vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa sababu miaka mingi ilienea shule za msingi na sekondari,” amesema Mahiza.

Vile vile, Mahiza ameahidi kufanikisha ujenzi wa kambi ya kimataifa ya Skauti jijini Dodoma.

“Wajibu wangu wa pili, ni kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa kambi ya kimataifa jijini Dodoma. Nakuahidi sitakuangusha,” amesema.


Mpekuzi.

Comments