Hayo aliyasema wakati akizungumza na Zanzibar Leo, mara baada ya utiaji saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na gesi.
Mkataba huo ulisainiwa juzi saa 1:57 usiku kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar (ZPDC), Mwanamkaa Abdulrhaman Mohamed na Mohamed Ataya, kutoka kampuni ya RAKGAS ya nchini Ras al Khaimah.
Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na Mtawala wa Ras al Khaimah, Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, Mawaziri wa SMZ na wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa chama.
Alisema kitendo chake cha kutoonesha upendeleo wa kutoa huduma muhimu katika jamii ya Wazanzibari, kimeonesha anavyowajali.
Alisema chama chao kimepokea kwa furaha tamko la kiongozi huyo kwani limewaonyesha njia ya kuwa na Zanzibar yenye maendeleo.
Zanzibarleo.
Comments