Wizara ya Afya yawatahadharisha wananchi kuhusu akaunti feki inayotumia jina la Waziri wa Afya Kutapeli Watu.
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
amekanusha vikali kuhusika na tangazo na umiliki wa ukurasa wa mtandao
wa Facebook wenye chapisho la matapeli wa mtandaoni linalotangaza ajira
za Shirika la Msalaba Mwekundu kwa watu 100 kila wilaya nchi nzima
lilioandikwa TANZANIA RED CROSS JOB APPLICATION FORM.
Ummy
Mwalimu kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika: “Huu ni UTAPELI,
Sihusiki na Sijui lolote kuhusu Kazi za Red Cross, na nimewaomba TCRA
kufuatilia na kuwachukulia hatua wahusika/matapeli hawa.”
Katika
tangazo hilo, muombaji wa ajira anatakiwa kutuma pesa kiasi cha Tsh.
10,000/= wanazodai kuwa ni za uanachama na kuzituma kupitia M-pesa namba
0767291550 (yenye jina la Mr. Shabu Lifumike, Ofisa Muajiri Mkuu).
Mpekuzi.
Comments