Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, ameahidi kumsomesha Wakonta Kapunda (26) ambaye
alipata ulemavu unaosababisha aandike kwa kutumia ulimi.
Wakonta ambaye ameishia kidato cha sita alipata ajali mwaka 2012 mkoani Tanga alipokuwa akienda katika sherehe za mahafali yake.
Akizungumza
jana wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Reginald Mengi
inayojihusisha na watu wenye ulemavu (DRMF), alisema atawasiliana na
familia ya binti huyo ili kumwezesha kutimiza ndoto zake.
“Serikali
inaheshimu na kulinda utu wa jamii mbalimbali wakiwamo watu wenye
ulemavu, tutaendelea kusimamia ulinzi imara kwa watu wenye ulemavu na
kuchukua hatua kali kwa yeyote atakaye wanyanyapaa na kuwaficha,”
alisema Majaliwa.
Pia
ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kutenga sehemu ya faida
wanazopata kusaidia watu wenye ulemavu kwa sababu suala la kuwahudumia
watu wenye ulemavu si la Serikali pekee bali jamii nzima.
Alisema
taasisi hiyo ni kielelezo muhimu cha mchango wa Dk. Mengi kwa watu
wenye ulemavu hapa nchini na kuwataka watu wengine waige mfano huo.
Naye
Dk. Mengi ameahidi kutoa Sh bilioni 5 kuwezesha ujenzi wa kiwanda kwa
ajili ya watu wenye ulemavu kitakachojengwa jijini Dar es Salaam.
“Usilalamike huna miguu au mikono bali tumia kikamilifu kile kilichobaki,” alisema Dk. Mengi.
mpekuzi.
Comments