Watendaji wa hifadhi ya msitu watakiwa kuwa wazalendo.

Image result for msitu wa ngezi pembaWafanyakazi na Wasimamizi wa hifadhi za misitu Zanzibar wametakiwa kuwa na moyo wa uzalendo katika kulinda na kuendeleza hifadhi ya misitu hiyo kwa maslahi ya Taifa na vizazi vya baadaye.

Mkurugenzi wa idara ya misitu na rasilimali zisizorejesheka Soud Moh’d Juma amesema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa si waadilifu na hushirikiana na wahalifu kwa kuharibu rasilimali na mazao ya misitu hiyo kitu ambacho kinaondoa haiba ya misitu hiyo.

Soud ameyasema hayo huko msitu wa Ngezi Kisiwani Pemba katika kikao cha pamoja kati wakuu wa idara ya misitu na wafanyakazi wa msitu huo.

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo amesema umefika wakati sasa kwa kila mhudumu wa hifadhi kutekeleza majukumu yake kwa vitendo ikiwemo kuandika taarifa za kazi alizozifanya kwa kutwa ili kuepukana na uhalifu huo.

Nao baadhi ya wafanyakazi hao wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika  utekelezaji wa shughuli zao ikiwemo kutokuwa na silaha, sare na vitambulisho vya kazi ambapo baadhi yao wamefika kuitishiwa usalama wao katika hatakati zao za doria.

Comments