Waliofariki dunia ajali ya kivuko cha MV Nyere wafikia 218....Mazishi Kufanyika Leo.

Miili 171 kati ya 218 iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.
 
Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jana  Jumamosi Septemba 22, 2018 saa 2 usiku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema wapo baadhi ya ndugu wanaotaka kuwazika wapendwa wao kisiwani humo.

Alisema kwa sasa taratibu mbalimbali zinafanyika, ikiwa ni pamoja na jitihada za kukinyanyua kivuko hicho kazi ambayo itafanywa na timu ya waokoaji.

“Kesho ( leo)  kuanzia saa 2 asubuhi kamati itafanya maziko ya miili 47,” alisema Mongella.

Miili iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.
 
Mpekuzi.

Comments