Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango nchini (TBS), zimetoa
ufafanuzi kuhusu vidonge vinavyodaiwa kuwapo kwenye chupa ya chai
ambavyo vinadaiwa kuwa na madhara kwamba si sumu na havina madhara kama
inavyodaiwa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo, vidonge hivyo si sumu
bali ni vitu vilivyotengenezwa kwa kutumia karatasi ambavyo ni
teknolojia ya kisasa inayotumika kutenganisha kuta mbili za chupa ili
kutunza joto la kimiminika kilichowekwa kwenye chupa husika.
“Hivi
karibuni kumekuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
kuhusu vidonge vilivyomo kwenye baadhi ya chupa za chai kuwa vidonge
vyenye dawa yenye madhara kwa watumiaji na video nyingine ya lugha ya
kiarabu ikieleza vidonge hivyo vina madini ya asbestos.
“Tunawahakikishia
wananchi kuwa bidhaa hizo ni salama kwa matumizi ya kutunza joto la
kimiminika kama vile chai,” imesema taarifa hiyo.
Pamoja
na mambo mengine, taasisi hizo zimeonya wananchi kuepuka kusambaza
taarifa kupitia mitandao ya kijamii zisizohakikiwa na taasisi hizo ili
kuondoa taharuki zisizo za lazima.
Mpekuzi.
Comments