Rais wa Zanzibar ateua Manaibu Makamo Wakuu wa Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar – SUZA.

uteuziRais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA amefanya uteuzi wa Naibu makamo mkuu wa chuo wa taaluma na Naibu makamo mkuu wa chuo wa Utawala. Rais Shein amemteua Dkt. Ali Makame Ussi kuwa Naibu Makamo Mkuu wa chuo taaluma na Dkt. Haroun ayoub Maalim kuwa makamo mkuu wa chuo Utawala.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya Uhusiano ya Chuo hicho iliyotolewa mapema leo asubuhi, Dkt. Ali Makame Ussi alikua ni Mkurugenzi anaeshughulikia masomo ya shahada ya awali chuoni hapo na Dkt. Haroun Ayoub Maalim alikua ni Mkuu wa Skuli ya Kiswahili na lugha za kigeni.
Dkt. Ussi alipata shahada ya kwanza na shahada ya uzamili katika masomo ya sayansi ya viumbe vya majini kutoka katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na Shahada ya uzamivu (PhD) kutoka katika chuo hicho hicho cha Dar es Salaam.
Nae Dkt. Maalim alipata Shahada ya mwanzo ya elimu kutoka Chuo kikuu cha SUZA , Shahada ya uzamili kutoka Chuo kikuu cha Melbourne na Shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes Afrika Kusini.
Uteuzi huu umefuatia kumalizika kwa muda wa uteuzi kwa aliekua naibu makamo mkuu wa chuo hicho upande wa taaluma Dkt. haji Mwevura Haji na Naibu Makamo Mkuu wa chuo upande wa Utawala Dkt. Zakia Mohamed Abubakar.
 Zanzibar24.

Comments