Baada
ya kumalizika kwa Uchaguzi wa ubunge Jimbo la Ukonga na Mwita Waitara
wa CCM kuibuka mshindi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro
Mambosasa kuitisha sherehe ya familia itakayowakutanisha askari -maarufu
kama polisi family day
Akizungumza
jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amempongeza Kamanda
Lazaro Mambosasa kwa kusimamia zoezi la uchaguzi wa Ukonga na maeneo
mengine ndani ya jiji hilo kwa kufanyika kwa amani.
“Kamanda
Mambosasa andaa polisi family day nataka iwe siku ya mfano Tanzania,
ili tupunguze msongo wa kazi ngumu mliyokua nayo wakati wa kulinda
amani ya Dar es salaam…”
Aidha
Paul Makonda amesema askari wa jeshi hilo watarajie kupata unafuu wa
gharama za ujenzi kufuatia kiongozi huyo kuzungumza na baadhi ya
wamiliki wa viwanda vya saruji pamoja na kiwanda cha Mabati ili
kuangalia namna ya kuliinua jeshi hilo.
Mapema
leo katika ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es salaam Msimamzi wa Uchaguzi
ilala Jumanne Shauri alimtangaza Mwita Waitara wa Chama cha Mapinduzi
kuwa mbunge mteule wa Ukonga kwa kupata jumla ya kura 77, 795 huku
mpinzani wake CHADEMA Asia Msangi akipata kura 8676.
Mpekuzi.
Comments