Mwanafunzi
wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Mbezi (19), Juma Idd jana
Jumatano Septemba 26, 2018 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la
tano mwenye miaka 14.
Mwanafunzi
aliyepewa ujauzito wenye miezi mitano sasa anasoma shule ya msingi
Kunduchi na tayari ameshaanza kliniki katika zahanati ya Tegeta.
Akisoma
shtaka hilo jana mbele ya hakimu Joyce Mushi, wakili wa Serikali Daisy
Makakala amedai tarehe tofauti kuanzia Aprili hadi Septemba mshtakiwa
alimwingilia kimwili mwanafunzi huyo huku ukijua ni kosa kisheria.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana kosa na wakili Makakala
aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika, kumuomba hakimu apange
tarehe nyingine.
Hakimu Mushi alimweleza mshtakiwa huyo kuwa dhamana yake iko wazi kwa kuwa shtaka hilo linalomkabili linadhaminika.
Hivyo
Hakimu Mushi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya
mwenyekiti wa serikali ya mtaa na kila mmoja atasaini bondi ya Sh1
milioni, masharti ambayo mshtakiwa huyo aliyatimiza na kuachiwa huru kwa
dhamana.
Mpekuzi.
Comments