Mwalimu
wa Shule ya Msingi Kisumba, Kalambo mkoani Rukwa, Lusekelo Mwakyesa
(47), amefariki dunia akiwa darasani wakati akisimamia mtihani wa darasa
la saba.
Tukio
hilo lilitokea juzi saa 9:30 alasiri katika Shule ya Msingi Mkapa
iliyoko katika kijiji cha Kateka, kata ya Matai wilayani Kalambo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alisema Septemba 3 majira ya
asubuhi, mwalimu huyo alikwenda katika kituo chake cha kazi na kuomba
ruhusa kwa Mwalimu Mkuu, Athuman Rashid, kuwa anahisi anaumwa malaria,
hivyo anataka kwenda kununua dawa.
Alisema
siku iliyofuata, mwalimu mkuu huyo alimuuliza mwalimu huyo kama ataweza
kwenda kusimamia mitihani ya darasa la saba katika kituo alichopangiwa
na kusema anaweza.
Aidha,
alisema siku hiyo mwalimu huyo alifika katika eneo ambalo wasimamizi
wote walielekezwa kufika ili wapewe maelekezo na waliulizwa kama kuna
msimamizi ambaye ana matatizo ya kiafya na hakuna aliyejitokeza, hivyo
walipelekwa katika vituo vyao.
Kamanda
Kyando alisema juzi Mwakyesa alifika katika chumba cha mtihani na
kuendelea kusimamia wanafunzi. Alisema asubuhi alimaliza mtihani wa
kwanza na kupumzika kwa ajili ya mtihani wa mchana.
Aliporudi
katika chumba cha mtihani, alisema mwalimu huyo alitoa maelekezo yote
kwa wanafunzi na kugawa karatasi za mitihani na za kujibia maswali na
alipomaliza alikwenda kukaa katika kiti alichoandaliwa ili apumzike huku
akiendelea kuwasimamia wanafunzi hao.
“Baada
ya kukaa, aliinama kama amejilaza katika meza iliyokuwa mbele yake kwa
muda mrefu bila kuinua kichwa ndipo mmoja wa wanafunzi, Joel Mwajungwa,
aliona maji yakitiririka kutokea miguuni kwa msimamizi huyo kitendo
kilicho mshtua na kutoka nje kumwita mgambo aliyekuwa akilinda usalama
katika maeneo ya shule,” alisema Kamanda Kyando.
Alisema
baada ya mgambo huyo kuingia darasani na kumtingisha, msimamizi huyo
hakuamka na alipoangalia yale maji alibaini kuwa ni haja ndogo na kutoa
taarifa kwa msimamizi mkuu aliyefika na gari na kumpeleka katika kituo
cha afya cha Matai kwa ajili ya matibabu.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kyando, walipofika kituo cha afya walipokewa na
mganga wa zamu, Chapanga Chapanga na alimfanyia uchunguzi na kubaini
kuwa alikwishafariki dunia.
Alisema
walipokagua katika begi lake walikuta dawa aina tano ambazo ni Aluu,
Panadol, Piriton, NTZ na Tsonizide na inasadikika kuwa mwalimu huyo
alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.
Mpekuzi.
Comments