Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amesema kivuko
cha Mv Nyerere kitapinduliwa chini juu hapo kilipo badala ya kuvutwa
hadi mwaloni kama mipango ya awali ilivyokuwa.
Jenerali
Mabeyo ametoa kauli hiyo jana, Septemba 23, 2018 eneo la Ukara wilayani
Ukerewe mkoani Mwanza baada ya kuwasili kifaa maalumu kitakachotumika
kukipindua kivuko kilichozama Septemba 20,2018 na kusababisha vifo vya
watu 224 hadi sasa.
“Tuombeni tufanikiwe na tutafanikiwa. Tunaamini kazi hii ya kukipindua kivuko hiki itaweza kuchukua siku mbili au tatu,”
“Kivuko
hiki kimejikita chini na kifaa hiki kitaingiza upepo utakaoingia kwenye
maboya yatakayosaidia kukipindua na hatua ya kukipindua itasaidia
kivuko hiki kutoharibika,” alisema Jenerali Mabeyo.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack
Kamwelwe alisema shughuli ya uokoaji inafanywa na Watanzania wenyewe na
si watu kutoka nje.
Pia,
amewapiga marufuku watendaji wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo
kukodi vifaa kwa ajili ya shughuli hiyo na kwamba kazi hiyo ipo chini ya
uratibu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Mpekuzi.
Comments