Mchekeshaji
mahiri Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ amesema watu wasipoteze muda wao
kufikiria kuna msanii atakayeweza kuziba pengo la mchekeshaji nguli
Bongo, marehemu Amri Athumani ‘King Majuto’, akisisitiza hilo
haliwezekani na kuongeza hata leo yeye akifariki dunia hakuna wa kuziba
pengo la Mboto.
“Ukweli
King Majuto ni yeye na mimi ni mimi niliona wakati alipofariki dunia
Kanumba, walikuja wanaofanana naye lakini si wasanii na wote waliotaka
kutembelea nyota ya Kanumba wamepotea,” alisema Mboto.
Mboto
anasema jambo la muhimu ni kuenzi mazuri ya King Majuto kwa kufanya
vizuri katika tasnia ya filamu na vichekesho na si kufanana na kumwiga
msanii mwingine.
Anasema
sanaa ni ubunifu kama yeye pamoja kuwa ni Mzaramo lakini watu wanaamini
ni Mkongo kwa jinsi anavyoigiza sauti za Kikongo.
Tufuatilie kupitia ........... https://www.youtube.com/channel/UCc_TYuIr0heTGwcQfHENDmA
Comments