Taasisi
na mashirika mbali mbali hapa nchini yametakiwa kurudisha sehemu ya
faida wanayo ipata ili kuhudumia Huduma za kijamii zikiwemo Mausala ya
afya elimu na watoto wasiojiweza Sanjari na maafa mbali mbali
Akizungumza
wakati akitoa msaada kwenye shule ya Msingi na ufundi Sing’isi wilayani
Arumeru mkoani Arusha mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa
Benki ya CBA bwana Julias Konyani amesema kwamba katika faida wanayo
ipata watakikisha wanaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini
Aidha
ameyataka mashirika mbali mbali kuona namna ya kurudisha faida
wanayopta katika kuhudumia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo
kusaidiana na serikali katika hatua mbali mbali za kuwaleta maendeleo
wananchi hususani benki hiyo ilipokuwa ikikabidhi hundi ya kiasi cha
shilingi milioni 4 katika shule ya msingi na ufundi ya Sing’isi
Amezitaka
taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuunga mkono jitihada za serikali
ya awamu ya tano ya ,kutoa elimu bure na kuwawezesha wanafunzi kupata
elimu ya awali bila kuwepo na changamoto ya madarasa pamoja na uhaba wa
vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusoma na kufundishia
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo ya Singisi Safira Ndelwa ametaja changamoto mbali
mbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya
majengo katika shule hiyo ikiwemo uhaba wa vyumba vya kusomea na uzio
wa shule
‘’Shule
hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uzio uhaba wa vyumba
vya madarasa mashine ya kuchapisha mitihani pamoja na nyumba za walimu
‘’alisema mwalimu Ndelwa
Mmoja
wa wanafunzi wa shule hiyo Anjela Izack ameshukuru benki hiyo kwa
msaada huo na kuomba kuongezewa madarasa mawili kwa lengo la kuondoa
usumbufu wa wanafunzi wenzake kusoma kwa awamu mbili kwani wanachoka na
masomo yao na kujikuta wakishindwa kushika masomo na maendeleo kushuka.
Pichani
ni Mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana
Julias Konyani akiwa na mwalim mkuu wa shule ya ufundi na msingi
Sing'isi Safira Ndelwa wakati wa makabidhiano ya Hundi kutoka Benki ya
CBA picha zote na mahamoud ahamd Meru
Sehemu
ya Wanafunzi wa shule ya msingi na ufundi Sing'isi wakiwa na mfano wa
hundi waliokabidhiwa na benki ya CBA jana wilayani Arumeru
Mpekuzi.
Comments