Baada
ya minada mitatu iliyofanyika kushindwa kupata mnunuzi wa makontena 20
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) sasa inafanya taratibu za kuyatoa bandarini ili kuyagawa
bure katika taasisi za kiserikali na pamoja hospitali..
Kamishana
Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema kuwa watayagawa bure hivi karibuni
kwani sheria inaruhusu kugawa katika taasisi za kiserikali na sio
binafsi pamoja na maeneo yoyote yenye huduma za kijamii, endapo mali
inapokosa mteja.
“Sheria
inaturuhusu kugawa popote kwenye huduma za kijamii ikiwemo hospitali,
kwakuwa minada yote hakuna mnunuzi aliyepatikana, kuna utaratibu
ulioelekezwa kisheria wa kuziondoa mali hizo sehemu ya mnada na moja ya
utaratibu huo ni kugawa bure”, amesema Kamishna Kichere.
Mara
ya kwanza makontena hayo yalipigwa mnada Agosti 25, lakini yalikosa
wanunuzi, watu wengi walishindwa kufikia bei iliyotakiwa, baadhi
wakitaja Shilingi milioni 10 kwa kontena badala ya Shilingi milioni 60
inayotakiwa, baaada ya makontena hayo kutouzika ambapo Agosti 26,
Makonda alitoa onyo akiwa mkoani Kagera kuwa atakayeyanunua atalaaniwa
yeye na uzao wake.
Agosti
27, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alikwenda bandarini
kuyakagua na kuwataka viongozi wenzake serikalini kutathmini kauli zao
na akawaomba wanaotaka kuyanunua wasiogope.
Akizungumza
na madiwani, viongozi na watumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato
mkoani Geita, Agosti 30, Rais John Magufuli alizungumzia sakata hilo
akiwataka viongozi kuwatumikia wananchi bila kujali wapo kwenye nafasi
gani.
“Umesikia
hili sakata la Dar es salaam, eti Mkuu wa Mkoa ameleta makontena,
ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe kodi?” Alihoji Rais Magufuli.
Sheria za nchi zinasema ni mtu mmoja katika nchi mwenye dhamana ya
kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya
dhamana na ya misaada.
“Sasa
ukichukua makontena kule umezungumza na watu wengine labda na
wafanyabiashara, unasema ni makontena yako halafu ukasema tena labda ni
ya walimu, wala hata shule hazitajwi maana yake nini”.
Chanzo:Eatv na Mpekuzi.
Comments